Jirani Yangu Tajiri

Wacha nkawasimlie ngano
Walakini si ngano ni hadithi
Maanake mimi ni muhusika
Katika hii hadithi

Kunaye huyu bwana mmoja
Aliyenunua jipande la shamba langu
Basi bwana huyo ni bwenyenye
Magari barazani
Ua la mawe na nyaya za umeme juu
Jumba la kufahari
Na kisha bango
" MBWA KALI "
Langoni

si mimi si mke wangu si watoto wangu
Tunaweza ingia kwenye hili kasri
Ingawa alikojenga bwana huyu
Tulipaita kwetu wakati mmoja
Ila sasa sisi wageni tu

Haya yote si hoja
Ya mno ni haya
Watoto wangu hawatacheza
Maanake wanatifua vumbi ikatwaa madirishani pake
Makelele ya wanangu chukizo
Eti mama mkubwa abarizi barazani

Na ukidhani mwisho hii lele tu
Jana nimewapata wanangu wakila uani
Kuuliza mbona, maanake si kawaida
Kitoweo cha nyama walinyimwa
Bahati nzuri harufu uani yafika

Maskini mimi ni hoi
Miliki yangu ni baiskeli kuu kuu
Ambayo nikaridhi kwa babu
Zaidi sina
Nifanyeje maanake masaibu sasa wimbo
Tangia nimpate jirani tajiri
Walau ningekuwa nimepangisha
Basi ningehama, lakini huku kwangu!

By wandez Mogire

Comments

Popular posts from this blog

Death You Are A Cheat