Wacha nkawasimlie ngano Walakini si ngano ni hadithi Maanake mimi ni muhusika Katika hii hadithi Kunaye huyu bwana mmoja Aliyenunua jipande la shamba langu Basi bwana huyo ni bwenyenye Magari barazani Ua la mawe na nyaya za umeme juu Jumba la kufahari Na kisha bango " MBWA KALI " Langoni si mimi si mke wangu si watoto wangu Tunaweza ingia kwenye hili kasri Ingawa alikojenga bwana huyu Tulipaita kwetu wakati mmoja Ila sasa sisi wageni tu Haya yote si hoja Ya mno ni haya Watoto wangu hawatacheza Maanake wanatifua vumbi ikatwaa madirishani pake Makelele ya wanangu chukizo Eti mama mkubwa abarizi barazani Na ukidhani mwisho hii lele tu Jana nimewapata wanangu wakila uani Kuuliza mbona, maanake si kawaida Kitoweo cha nyama walinyimwa Bahati nzuri harufu uani yafika Maskini mimi ni hoi Miliki yangu ni baiskeli kuu kuu Ambayo nikaridhi kwa babu Zaidi sina Nifanyeje maanake masaibu sasa wimbo Tangia nimpate jirani tajiri Walau ningekuwa nimepan...
Comments
Post a Comment